JOHANESBURG, Afrika Kusini.
TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania "Twiga Stars" wamezidi kujiweka katika nafasi ngumu ya kusonga katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mali.
Kama sio makosa ya mlinda mlango wa Tanzania Jawadu Omari katika mchezo huo wa pili katika kundi A, ambapo tulishuhudia mabadiliko ya hali ya hewa na kusababisha mashabiki kukimbia uwanjani.
Bao la kwanza la Mali lilifungwa katika dakika 25 na mchezaji Konate Aicha kwa mpira wa adhabu uliopigwa umbali wa mita 40 uliotiga moja kwa moja wavuni, bao hilo liliongeza morali kwa wachezaji wa Mali na kufanya wawe wanajaribu mashuti ya mbali mara kwa mara.
Nahodha wa timu ya Twiga Mwasikili Edward alisawazisha bao hilo dakika ya 30 baada ya kupokea mpira wa adhabu ulipigwa na kugonga ukuta wa Mali na kumkuta yeye na kuutumbukiza nyavuni.
Bao la pili la Mali lilifungwa na Diarra Fotounata dakika ya 32 kabla ya bao hilo kusawazishwa na Esther Chabruma dakika moja baaye na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
Bao la tatu la Mali lilifungwa dakika ya 57 na Nohodha wake N'diaye Diaty kwa shuti la mbali, bao ambalo lilididimiza ndoto za Twiga Stars kusonga mbele.
Twiga Stars inatarajiwa kucheza mchezo wake mwisho Jumapili dhidi ya mabingwa watetezi Nigeria ambao waliwafunga wenyeji Afrika Kusini mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment