Friday, November 5, 2010

DROGBA AWAONYA WENZAKE KUHUSU MCHEZO WAO DHIDI YA LIVERPOOL.

LONDON, England
MASHAMBULIAJI wa Chelsea Didier Drogba amewasihi wachezaji wenzake wasibweteke kwa kudhani mchezo dhidi ya Liverpool unaowakabili utakuwa mwepesi.

Mshambuliaji huyo alisema wakati timu hiyo itapofunga safari Jumapili hii kwenda Anfield kuikabili timu hiyo ambayo msimu huu imekuwa ikisuasua kwani mpaka sasa imeshinda mechi mbili kati ya tisa ilizocheza katika Ligi Kuu ya nchi hiyo huku wao wakiwa wanaongoza ligi hiyo.

"Haitakuwa mechi rahisi kwani watataka kuendeleza wimbi la ushindi ili kuhakikisha wanapanda juu haswa ikizingatiwa kuwa watakuwa nyumbani." alisema Drogba.

No comments:

Post a Comment