Friday, November 5, 2010

KIBARUA CHA MANCINI HATARINI.

LONDON, England
MANCHESTER City jana walikubali kipigo kingine cha mabao 3-1 kutoka katika timu ya Lech Poznan katika mchezo wa Kombe la Uefa.

Kipigo hicho kinaweza kikawa mlango wa kutokea kwa kocha wa City Roberto Mancini ambapo kumekuwa na fununu za chini kwa chini kwamba wachezaji wa timu hiyo hawamkubali.

City imekuwa ni timu iliyotumia mapesa mengi katika usajili katika kipindi cha majira ya kiangazi hivyo vipigo mfululizo wanavyovipata lazima vitakuwa vinamuweka pabaya Mancini.

Suala la Mancini litajulikana wazi baada ya mechi dhidi ya wapinzani wao Manchester United mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumatano Novemba 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment