Saturday, November 6, 2010

WENGER ASHANGAZWA KUITWA KWA VAN PERSIE TIMU YA TAIFA.

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger ana wasiwasi kufuatia mshambuliaji wake Robin Van Persie kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.

Wenger alisema Alhamisi kushangazwa kwake na kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk kwa uamuzi wake wa kumuita mchezaji huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ndio kwanza ameanza mazoezi hivi karibuni baada ya kuumia kifundo cha mguu mwishoni mwa mwezi Agosti, na anasema kuwa itakuwa ni sahihi kama asipomruhusu mchezaji huyo.

"Kwa sasa, Robin va Persie ndio amerudi baada ya kuumia, sisi wenyewe tuna wasiwasi wa kumtumia katika klabu yetu na unaweza kuelewa ni jinsi hatutapenda pia acheze katika mchezi huo wa kirafiki na timu ya Taifa," alisema Wenger.

No comments:

Post a Comment