Saturday, November 6, 2010

MARADONA ATIMKIA IRAN.

DIEGO Maradona anaweza akapewa nafasi ya kuifundisha timu ya Taifa ya Iran kwa mujibu wa gazeti la moja la michezo nchini humo.

Rais wa Shirikisho la Soka la Iran (FFIRI) Ali Kaffashian alitarajiwa kuongea na Maradona. Wakala wa kocha huyo alitegemewa kutembelea Iran Jumamosi kabla ya kuanza kwa mazungumzo.

Maradona pia alisema alimtumia jezi yake Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.

No comments:

Post a Comment