Tuesday, November 9, 2010

PAULSEN ATAJA KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS.

KOCHA wa timu ya soka ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" Jan Poulsen leo ametaja kikosi cha timu hiyo kitachoiwakilisha Tanzania katika michuano ya CECAFA Tusker Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Paulsen alisema katika kikosi hicho kitawakilishwa na majina kama ifuatavyo:

Makipa: Juma Kaseja, Shaban Kado na Said Muhando.

Mabeki: Shadrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasika, Haruna Shamte na Idrissa Rajabu.

Viungo: Juma Nyoso, Shaaban Nditi, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Jabir Aziz, Nizar Khalfan, Meshack Abel, Mohamedi Banka na Kigi Makasi.

Washambuliaji: Dany Mrwanda, Mrisho Ngassa, John Boko, Thomas Ulimwengu na Gaudence Mwaikimba.

Poulsen alisema baadhi ya wachezaji hao pia wataunda kikosi cha timu ya taifa "Taifa Stars" kitakachocheza mechi ya taifa ya kirafiki Novemba 17 kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika baadae mwakani itakayofanyika Gunea.

No comments:

Post a Comment