ABU DHABI
MSHAMBULIAJI wa Inter Milan amesema kuwa anafuatilia kiwango cha wawakilishi wa Afrika TP Mazembe katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kwa kujivunia kwa kiasi kikubwa.
Nilifuatilia toka mechi yao ya kwanza nilipowasili Abu Dhabi," alisema nahodha huyo wa Cameroon akiongea na mtandao wa FIFA.com Jumatano.
Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pachuca ulivyoanza na tayari walikuwa wameshashinda. Waafrika katika timu yetu walianza kuwapa moyo, wakiwamini kuwa watashinda.
Nilifurahi na kujivunia kwa kuwa walishinda mchezo huo. Wanajivunia kuliwakilisha bara letu, baada ya ushindi katika mchezo wao wa pili dhidi Internacional kutoka Amerika Kusini na napenda kutuma salamu za pongezi kwao."
Inter nao walifanikiwa kuingia fainali Jumatano baada ya kuifunga klabu ya Seongnam kutoka Asia mabao 3-0. Sasa watakutana na TP Mazembe katika mchezo wa fainali Jumamosi usikose.
No comments:
Post a Comment