ZURICH, Switzerland
HISPANIA ambayo imeshinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka huu inamaliza mwaka ikiwa inaongoza katika viwango vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Uholanzi ambayo ilifungwa katika fainali za Kombe la Dunia na Hispania inashika nafsi ya pili wakati Ujerumani imepanda nafasi moja juu ya Brazil ambayo inashika nafasi ya nne toka mwezi uliopita. USA ndio inaongoza nchi za Amerika Kaskazini (CONCACAF), huku kwa upande wa viwango vya FIFA ikipanda kwa nafasi sita hadi nafasi ya 18.
Argentina na England zimebaki katika nafsi zao ya tano na sita. Hispania wameongoza katika orodha hiyo ya viwango vya FIFA kwa miaka mitatu mfululizo.
Nchi pekee ya Afrika iliyopo katika kumi bora Misri wao wamepanda nafsi moja hadi ya tisa, wakati Australia imeshuka kwa nafasi sita hadi ya 26 lakini bado inashikilia nafasi ya kwanza kwa nchi za Asia.
Urusi ambayo imeshinda nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia 2018 mapema mwezi huu imebaki katika nafasi ya 13 wakati wenyeji wa fainali hizo 2022 Qatar wameanguka mpaka nafasi ya 114.
No comments:
Post a Comment