ABU DHABI.
KOCHA wa TP Mazembe Lamine N'Diaye ameonyesha kufurahishwa kwake baada ya ushindi walioupata wa mabao 2-0 dhidi ya Internacional katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Klbu Bingwa ya Dunia ulichezwa usiku huu.
Ni mara ya kwanza kwa timu ya Afrika kufika katika hatua hiyo katika mashindano hayo na N'Diaye anajivunia kwa kiasi kikubwa uwezo walionyesha wachezaji wake.
"Ni kitu muhimu kwetu," alisema N'Diaye akiuambia mtandao wa Fifa.com. Tupo hapa kuiwakilisha Afrika, na Afrika nzima itajivunia kazi yetu.
"Tunajiamini, tuna uhakika na unaweza kuona kuona hilo wakati tukianza kushambulia, haswa mwanzoni mwa kipindi cha pili. Tuna bahati pia, na usisahau golikipa wetu ni mzuri ni kama mchawi vile!
"Tumefanikiwa kuonyesha kwamba wachezaji wetu ni wa kiwango cha juu. Tumepata ushindi mzuri. Ni ushindi mzuri kwa timu na watu wa DRC, na kila mwafrika anapaswa kujivunia timu hii."
Mazembe sasa anasubiri kukutana na mshindi katika fainali kwenye mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya aidha Inter Milan au Seongnam IIhwa Chunma mchezo utakachezwa leo.
No comments:
Post a Comment