Wednesday, December 29, 2010

LEONARDO ATWAA MIKOBA INTER.

MILAN, Italia
KOCHA wa zamani wa AC Milan Leonardo ameajiriwa kama kocha mpya wa Inter Milan.

Mabingwa hao wa Ulaya na Italia walimtaja kocha huyo katika mtandao wake Ijumaa, siku baada ya mkataba wa Rafa Banitez haujasitishwa.

Mkataba wa Leonardo unaanza Jumatano na unafikia tamati June 2012.

Benitez ameingoza Inter kunyakuwa ubingwa wa Klabu Bingwa ya Dunia wiki iliyopita, lakini timu inashikilia nafasi ya saba katika ligi, wakiwa pointi 13 nyuma ya mahasimu wao AC Milan wanaongoza ligi hiyo. Kocha huyo wa Hispania amedumu katika klabu hiyo kwa muda wa miezi sita baada ya kuchukua mikoba iliyoachwa na Jeso Mourihno, aliyeondoka kuelekea Real Madrid msimu huu.

No comments:

Post a Comment