Wednesday, December 29, 2010

AJALI YA PIKIPIKI YAMUONDOA DUNIANI MCHEZAJI WA ZAMANI WA LIVERPOOL.

MCHEZAJI wa kimataifa wa zamani wa Israel na Liverpool Avi Cohen amefariki dunia kufuatia majeraha makubwa aliyopata kichwani baada ya kupata ajali ya pikipiki.

Mtoto wa kiume wa mchezaji huyo Tamir Cohen anayechezea klabu ya Bolton Wanderers katika ligi kuu ya Uingereza amesema baba yake alitangazwa kufariki na madaktari katika hospitali ya Ichilov mjini Tel Aviv.

Avi Cohen aliyekuwa akicheza nafasi ya ulinzi alikuwa mchezaji wa kwanza wa Israel kucheza katika ligi kubwa ya Uingereza wakati alipojiunga na klabu ya Liverpool mwaka 1970.

Baada ya kustaafu kucheza soka Avi Cohen aliyefariki akiwa na umri wa miaka 54, alikuwa mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa kulipwa cha Israel kwa zaidi ya miaka mitano hadi wakati mauti yalipomkuta.

No comments:

Post a Comment