Tuesday, December 28, 2010

WALCOTT: TULISTAHILI KUSHINDA.

LONDON, England
WINGA machachari wa Arsenal Theo Walcott kuwa ana furaha kubwa mara baada ya kuwafunga Chelsea katika Uwanja wa Emirates na kuifanya timu ikwee mpka akatika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya magoli mbele ya Manchester City.

Alex Song ndio aliyefunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya mabao kutoka kwa Walcott na Cesc Fabrigas na kuifanya timu kuongoza mabao 3-0. Branislav Ivanovic alifunga bao la kufutia machozi la Chelsea.

Akiongea na Sky Sports baada ya mchezo Walcott alisema timu yake ilionyesha uwezo mkubwa katika kuzuia lakini aliwaonya wachezaji wenzake kuendelea kucheza kiwango hichohicho katika mchezo wao dhidi ya Wigan Athletic Jumatano usiku.

No comments:

Post a Comment