ARGENTINA
MSHAMBULIAJI wa Barcelona Lionel Messi amewasili Argentina ambako atasherekea sikukuu ya Xmas na familia yake.
Waandishi wa Habari walikuwapo katika Uwanja wa ndege wakati alipotua nchini kwao huko, na aliongea nao kuhusu mustakabali wa msimu huu wa ligi huko Hispania pamoja na tuzo zinazokuja za mchezaji bora wa dunia.
"Mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka mzuri kwa mimi binafsi, lakini Kombe la Dunia halikwenda kama tulivyotaka," alisema Messi.
"Sasa nina majukumu ya kuhakikisha Argentina inashinda Copa America mwaka ujao, ikizingatiwa itakuwa ikichezwa hapa nyumbani.
Alipoulizwa kuhusu mawazo yake ya nani atashinda Ballon d'Or tuzo ambayo ndio nayoshikilia hivi sasa aliwapigia chapuo wachezaji wenzake wa Barcelona ambao wapo wote katika kinyang'anyiro hicho.
"Mwaka huu nafikiri mmoja kati ya wachezaji wenzangu, Xavi au Iniesta, mmoja wao anaweza kushinda," alisema.
Viungo hao wawili ni miongoni kati ya wachezaji watatuwanaogombea tuzo huyo, huku wa tatu akiwa ni Messi mwenyewe.
No comments:
Post a Comment