Monday, January 17, 2011

BABEL ATOZWA FAINI

Picha ya mwamuzi Howard Webb akiwa amevaa jezi ya Man United ambayo imemtia matatani Babel.

LONDON, England
Winga machachari wa Liverpool Ryan Babel amepigwa faini ya dola 16,000 na Shrikisho la Soka la Uingereza kwa kutoa comment za kuponda marefa wanaochezesha Ligi Kuu ya Uingereza katika mtandao wa Twitter.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uholanzi alituma picha katika mtandao huo ya mwamuzi Howard Webb akiwa amevaa jezi ya Manchester United baada ya kuchukizwa na maauzi aliyiyafanya katika mchezo ambao timu hiyo ilipoteza kwa United kwa kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Old Traford Jan 9, 2011.

No comments:

Post a Comment