LONDON, England
David Beckham amefanyiwa vipimo katika klabu ya Tottenham Jumatatu hii kabla ya kuanza mazoezi na klabu hiyo.
Pamoja na mchezaji huyo kupata ruksa ya kuchezea klabu hiyo kwa miezi miwili kwa mkopo kutokea Los Angeles Galax, kiungo huyo na Spurs wanaamini kwamba wataweza kuongeza mkataba huo.
Baada ya kufanyiwa vipimo katika Uwanja wa mazoezi wa Spurs Mashariki mwa London, Beckham aliondoka ndani ya masaa mawili akkiwa amevaa traki-suti ya klabu hiyo.
Beckham (35) ana matumaini ya kuichezea Tottenham ili kufufua matumaini yake ya kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza, ambapo mpaka sasa ameshaitwa mara 115 akiwa ndiye mchezaji aliyechezea mechi nyingi timu hiyo ya taifa.
No comments:
Post a Comment