ZURICH, Uswis
Lionel Messi ameshinda tuzo ya pili ya mchezaji bora wa dunia, na amekuwa mchezaji wa kwanza kupata tuzo hiyo mfululizo toka aliposhinda Ronaldinho mwaka 2004-2005.
Mshambuliaji huyo wa Argentina amewashinda wachezaji wenzake anaocheza nao katika timu ya Barcelona Xavi Hernandez na Adres Iniesta katika tuzo hizo.
Mchezaji mwanamama Marta ameshinda tuzo kama hiyo kwa upande wa kina mama kwa mwaka wa tano sasa.
Jose Mourinho Kocha wa Real Madrid amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka baada ya kuingoza Inter Milan kushinda taji la Champions League.
Messi (23) ameisaidia Barcelona kutetea taji lake la ligi ambapo mpaka sasa pia wwanaongoza ligi ya Hispania.
Mourinho ameisaidia Inter kushinda mataji matatu mfululizo kabla ya kujiunga na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment