BRAZIL
KLABU ya soka ya Flamengo ya Brazil imeweka wazi katika mtandao wake kwamba imemsajili kiungo nyota Ronaldinho kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.
AC Milan klabu ya zamani ya Ronaldinho itakuwa italipwa kiasi cha Euro milioni 3 kwa uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Rossoneri kwenda Mengao, na atakuwa akilipwa kiasi cha Euro 130,000 kwa wiki, kiasi ambacho kitakuwa kikilipwa na na wawekezaji wa timu hiyo Traffic na Olympikus.
Mchezaji huyo wa zamani wa mwaka wa FIFA anatarajiwa kutangazwa rasmi katika vyombo vya habari Alhamisi.
No comments:
Post a Comment