Thursday, January 20, 2011

DONDOO ZA DIRISHA DOGO UINGEREZA.

LONDON, England
Wakati dirisha dogo la usajili likiwa wazi katika ligi kuu ya Uingereza, klabu za Arsenal na Manchester United zimesemekana kumuwania mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos.

Beki huyo wa kimataifa wa Hispania anawaniwa kwa kitita cha paundi milioni 25.

Wakati huo huo wachezaji wawili wa klabu ya Everton wenye umri wa miaka 22 Victor Anichebe na Seamus Coleman kwa pamoja wametia saini mikataba mipya ya miaka minne na nusu kila mmoja kuendelea kusaka kabumbu katika klabu hiyo.

Naye Bosi wa klabu ya Sunderland Steve Bruce anatazamiwa kuzungumza na meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson kuhusiana na suala la kumsajili nyota wa Manchester United Michael Owen mwezi huu.
Bosi huyo wa ‘The Black Cats’ anafanya jitihada za kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuziba nafasi ya Darren Bent aliyetimka na kujiunga na Aston Villa.

No comments:

Post a Comment