Monday, January 31, 2011

KILI MARATHON YAPAMBA MOTO.

Picha inawaonyesha wakimbiaji wakianza mbio za mashindano hayo mwaka jana.

MOSHI, Kilimanjaro
MITAA ya mji wa Moshi inatarajiwa kufurika watu watakajitokeza kushuhudia mbio kubwa barani Afrika hapo siku ya Jumapili tarehe 27 Februari 2011, wakati maelfu ya wakimbiaji watakaposhiriki mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Marathon.

Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Francis John alisema mbio hizo zitashirikisha wanariadha nyota barani Afrika waliowahi kuvuma kitaifa na kimataifa.

Mlima Kilimanjaro.

Amewataja baadhi ya wanariadha hao kuwa ni pamoja na Patrick Nyangero, Andrea Silvini, Daudi Joseph, Sarah Majah, Sarah Kavina na Banuelia Brighton.

No comments:

Post a Comment