Monday, January 31, 2011

LEE AFURAHIA BAO ALILOFUNGA KATIKA MCHEZO WA FAINALI DHIDI YA AUSTRALIA.

DOHA, Qatar
SHUJAA wa Japan katika mchezo wa fainali wa Kombe la Bara la Asia dhidi ya Australia, Tadanari Lee amefurahishwa kwea kushinda bao lake la kwanza akiwa na Blue Samurai katika mchezo muhimu katika mashindano hayo.

Ilimchukua dakika sita toka lipoingia uwanjani kufunga bao hilo la ushindi, ambalo liliiongoza timu hiyo kutawazwa mabingwa wapya wa michuano ya hiyo katika bara la Asia.
"Nilikuwa nataka kwenda upande wa karibu lakini nilimuona beki wao akienda upande ule. Hivyo nilisimama na Nagamoto akanipa mpira mzuri. Wakati mpira uliponifikia nilifikiria kuwa nahitaji kuupiga," alisema Lee akihijiwa na mtandao goal.com

Akiwa pia amekwisha ichezea timu ya Korea Kusini ya chini ya miaka 20 mwaka 2004, Lee (25) anafurahia kuifungia Japan kwa staili ya aina yake.

"Nimekulia katika utamaduni wa kijapan na napenda nchi zote yaani Korea na Japan. Nimefurahi kuifungia bao Japan," alisema Lee.

No comments:

Post a Comment