Pichani hapo ni Obilale golikipa wa Togo akiwa amelala kitandani akikimbizwa hospitalini mara baada ya kutua nchini Afrika Kusini.
LUANDA, Angola
MAHAKAMA nchini Angola imemhukumu mtu mmoja miaka 24 jela kufuatia tukio la kushambulia msafara wa timu ya Taifa ya Togo mapema mwaka jana shambulio ambalo lilipelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine nane kujeruhiwa, akiwemo golikipa namba moja wa timu hiyo.
Jean Antuan Pwaty (42) raia wa Congo DRC alihukumiwa kwa makosa matatu la kuuwa, kumilikisilaha kinyume cha sheria na shambulio la mauaji iliripoti redio moja nchini Angola. Mwanasheria wake amesema atakata rufani kufuatia adhabu aliyopewa mteja wake huyo.
Obilale akiwa katika baiskeli ya magurudumu nchini Ufaransa akitibiwa ili aweze kutembea tena, lakini ndoto za kucheza tena soka hazipo kwa mchezaji huyo.
Timu ya Taifa ya Togo kutoka upande wa Magharibi mwa Afrika ilikuwa ikisafiri kwa barabara kuelekea kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yalifanyika Angola Januari mwaka jana wakati basi lao walilokuwa wakisafiria kushambuliwa kwa risasi katika mji wa Cabinda uliopo mpakani mwa Angola.
Kocha wa timu ya Togo na mwandishi wa habari waliuawa katika tukio hilo. mmoja ya walijeruhiwa golikipa Kodjovi Obilale, ambaye alipata majeraha kiunoni alisema hategemei kucheza mpira tena kwa majeraha aliyopata lakini ana matumaini ya kutembea siku kwani mpaka hivi sasa bado hawezi kutembea.
No comments:
Post a Comment