Tuesday, January 4, 2011

TAIFA STARS KUIVAA MISRI KATIKA NILE BASIN FRIENDLY TOURNAMENT.

CAIRO, Misri
TIMU ya Taifa ya Misri itacheza mchezo wake ufunguzi na timu ya Taifa ya Tanzania katika michuano ya kirafiki ya Nile Basin Januari 5 mwaka huu. Michuano hiyo imeandaliwa na Misri kuanzia Januari 5 mpaka 7 na inatarajiwa kushirikisha nchi 7 za Afrika. Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Sudan, Tanzania, Uganda, Burundi, Kenya, Congo DR na wenyeji Misri. Lengo kubwa la michuano hiyo ni kuunda umoja na kulinda vyanzo vya Mto Nile kwa ajili ya kizazi kijacho ambapo nchi zote hizo zinazoshiriki zinatumia mto huo.

Nchi nne, Misri, Tanzania, Uganda na Burundi zitacheza katika kundi A, wakati kundi B zitakuwepo nchi za Sudan, Kenya na Congo DR.

Katika droo iliyochezeshwa iliiweka Uganda na Sudan tofauti baada ya Sudan kuomba wasichezeshwe kundi moja na Uganda ambao wanakutana nao katika kundi moja katika michuano ya CHAN 2011 mwezi ujao.

Timu mbili kutoka katika kila kundi ndizo zitafuzu hatua ya nusu fainali. Ambapo timu itakayoongoza katika kundi A itacheza na timu itayoshika nafasi ya pili ya kundi B, wakati timu itakayoongoza kundi B itacheza na timu itayoshika nafsi ya pili katika kundi A.

Timu zitakazoshika nafasi ya tatu katika makundi hayo mawili zitashindania nafasi ya tano.

No comments:

Post a Comment