LONDON, England
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Luis Nazario de Lima hii leo ametangaza rasmi kustahafu soka baada ya kuutumikia mchezo huo kwa muda wa miaka 24 iliyopita.
Mshambuliaji huyo anaeshikilia rekodi ya kupachika mabao mengi kuliko mchezaji yoyote aliewahi kucheza fainali za kombe la dunia toka ziazishwe mwaka 1930, amefikia maamuzi ya kustahafu soka kwa sababu mbili tofauti ambapo sababu ya kwanza ni kutaka kupata muda wa kufanya shughuli nyingine za kimaisha ambazo amedhamiria kuzifanya.
Amesema muda mrefu amekua akiutumikia mchezo wa soka pasipo kujishughulisha na shughuli za kimaisha ambazo kwa kipindi kirefu amekua akizifanya kwa kujiibia muda wake na kwa sasa ameona muda umefika kuingia katika utaratibu huo moja kwa moja.
Sababu ya pili amedai ni kuzidiwa na mwili ambao kwa sasa ni mkubwa zaidi ya alivyokua siku za nyuma.
Hata hivyo ameeleza kwamba bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu yake ya sasa ya Corinthians ya nchini Brazil ambayo ilimsajili kutoka Ac Milan ya nchini Italia mwaka 2009 lakini ameona ni bora akae pembeni na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kuonyesha uwezo wao.
Ronaldo Luis Nazario de Lima ambae amepachikwa majina mengi kama R9, The Phenomenon pamoja na The Big ataendelea kukumbukwa kwa uwezo wake binafsi wakati alipokua akivitumikia vilabu kama Cruzeiro, PSV, Barcelona ,Inter Milan, Real Madrid, AC Milan na Corinthians ambao ulimuwezeshwa kutwaa tuzo ya uchezaji bora dunia mara tatu ambapo hiyo ilikua mwaka 1996, 1997, 2002.
Akiwa na timu ya taifa ya Brazil kuanzia mwaka 1994–2006 alifanikiwa kucheza michezo 97 na kupachika mabao 62 huku akitwaa ubingwa wa dunia mara mbili mwaka 1994 na mwaka 2002.
HIZI NDIO TUZO ALIZOFANIKIWA KUTWAA WAKATI WA UCHEZAJI WAKE.
* Supercopa Libertadores Top Scorer: 1993–94
* Campeonato Mineiro Top Scorer: 1993–94
* Campeonato Mineiro Team of The Year: 1994
* Eredivisie Top Scorer: 1994–95
* La Liga Top Scorer: 1996–97,2003–2004
* European Golden Boot: 1996–97
* Don Balón Award La Liga Foreign Player of the Year: 1996–97
* Copa América Final Most Valuable Player: 1997
* Copa América Most Valuable Player: 1997
* Confederations Cup All-Star Team: 1997
* Cup Winners Cup Final Most Valuable Player: 1997
* Cup Winners Cup Top Goal Scorer: 1996–1997
* IFFHS World's Top Goal Scorer of the Year: 1997
* UEFA Most Valuable Player: 1997–98
* Serie A Footballer of the Year: 1997–98
* Serie A Foreign Footballer of the Year: 1997–98
* UEFA Best Forward: 1997–98
* Bravo Award : 1995, 1997, 1998
* FIFA World Cup Golden Ball: 1998
* UEFA Cup Final Most Valuable Player: 1998
* Copa América Top Scorer: 1999
* Copa América All-Star Team: 1997, 1999
* FIFA World Player of the Year: 1996, 1997, 2002
* Ballon D'or: 1997, 2002
* World Soccer Magazine World Player of The Year: 1996,1997.2002
* Onze d'Or: 1997, 2002
* FIFA World Cup Silver Ball: 2002
* FIFA 100
* FIFA World Cup All-Star Team: 1998, 2002
* FIFA World Cup Final Most Valuable Player: 2002
* FIFA World Cup Top Scorer: 2002
* Intercontinental Cup Most Valuable Player: 2002
* UEFA Team of The Year: 2002
* Laureus Comeback of the Year: 2002
* Strogaldo De Legendary Award 2002
* BBC Sports Personality of the Year Overseas Personality: 2002
* La Liga South American Player of the Year: 1996–97, 2002–03
* Golden Foot award: 2006
* Brazilian National Hall of Fame: Class of 2006
* Serie A Player of the Decade: 1997–2007
* France Football Magazine: Starting eleven of all-time (2007)
* FIFA World Cup: All-Time Leading Scorer
* Campeonato Paulista: Best Player, 2009
* Goal.com : Player of a decade: Winner 2000–2010[27]
No comments:
Post a Comment