TIMU ya Villa squad yenye makazi yake jijini Dar es Salaam imefanikiwa kurejea katika Ligi kuu ya soka Tanzania baada ya kutoka suluhu na timu ya Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi ya Daraja la Kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Villa Squad imefikisha pointi 12 sambamba na Polisi Morogoro, lakini timu hiyo ya Magomeni iliyoshuka daraja mwaka 2009, inafaida ya tofauti ya magoli, ambapo ina magoli 12 ya kufunga dhidi ya magoli 8 ya Polisi Moro.
No comments:
Post a Comment