![]() |
Pep Guardiola |
LONDON,England
”KOCHA wa Barcelona Pep Guardiola anatarajiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo Jumatano alisema mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
Ilitangazwa mapema mwezi huu kuwa Guardiola atasaini mkataba mpya Jumanne lakini sasa imerudishwa nyuma kwa masaa 24.
“Mapema ilitangazwa kuwa kocha huwa natakiwa kusaini mkataba wake mpya Jumanne Februari 22, lakini sasa imeamualiwa kuwa atasaini mkataba huo Jumatano Februari 23, baada ya mazoezi ya timu hiyo,” ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.
“Guardiola atasaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja mpaka Juni 30,2012, ilitangazwa Februari 8.”
Guardiola (40) alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwaka 2008 na tayari ameiwezesha klabu hiyo kushinda mataji 8. Ambapo alieleza nia yake ya kuendelea kuinoa klabu hiyo mwezi Januari, na uongozi wa Barca ulitoa taarifa ya kumuongeza mkataba mapema Februari.
“Kwa kocha, baada ya kipindi fulani mambo kama hayo yanakuwa ya kawaida kwake na wakati huo ukifika lazima ujue jinsi ya kuepukana nayo,” alisema Guardiola. “Lakini bado muda mwingi umebakia katika mkataba wangu na klabu inajua siwezi kuwaacha, hivyo naomba nifanhye kazi yangu kwa amani.”
No comments:
Post a Comment