Monday, February 21, 2011

"TUMEJIONGEZEA MCHEZO USIO WA LAZIMA." WENGER.

LONDON, England
SIKU moja baada ya kung’ang’aniwa na klabu ya Leyton Orient kwa kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja kwenye mchezo wa michuano ya kuwania ubingwa wa kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA, meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Charles Ernest Wenger amesema matokeo hayo yamewalazimisha kujiongezea mchezo ambao ulikua hauna ulazima wa kuwepo.

Wenger amesema mchezo huo umewaongezea michezo zaidi ya ile wanayoifikiria kwa sasa kutokana na sheria ya michuano ya kombe la FA kuwalazimisha kucheza tena dhidi ya Leyton Orient huko Emirates kwa lengo la kumsaka mshindi atakaetinga kwenye hatua ya robo fainali.

mzee huyo pia amebainisha kwamba kiujumla kikosi chake kilicheza kwa kujituma wakati wote lakini makosa madogo madogo waliyoyafanya dakika za lala salama yaliwagharimu na kutoa nafasi kwa wapinzani wao kusawazisha kupitia kwa Jonathan Kahne Téhoué.

Hata hivyo Arsene wenger amekimwagia sifa kede kede kikosi cha Leyton Orient kufuatia kuonyesha soka safi na lenye kutokatisha tamaa licha ya upande wa Arsenal kupata bao katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili lililofungwa na Thomas Rosicky.

No comments:

Post a Comment