Monday, February 21, 2011

"MODRIC IS NOT FOR SALE," REDKNAPP.

Luka Modric
LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema hatomuuza kiungo Luka Modric ambaye kwa sasa anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Man Utd.

Harry Redknapp amekataa kuingia kwenye biashara ya kumuuza kiungo huyo kufuatia uvumi unaomuhusu yeye kuwa tayari kufanya hivyo kuendelea kushamiri kwenye vyombo mbali mbali vya habari ambapo amesema uvumi huo ni mzushi mtupu.

Alisema hata yeye amekua akizisikia taarifa hizo za Luka Midric kuwa mbioni kuuzwa na klabu yake huku ikielezwa tayari dau la paund million 35 limeshatengwa kwa ajili ya safari yake ya kuelekea huko Old Trafford yalipo makao makuu ya klabu ya Man Utd.

Alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekua na maendeleo mazuri ndani ya kikosi chake toka aliposajiliwa huko White Hart Lane mwaka 2008 akitiea kwenye klabu ya Dynamo Zagreb hivyo haoni sababu ya kulazimika kumuondoa kwa sasa wakati bado Spurs inamuhitaji.

Redknapp akaendelea kumsifia mchezaji huyo kwa kusema ni msikivu na wala hapendi makuu, zaidi ya kutaka kucheza soka wakati wote hali ambayo inamfanya apendwe na wachezaji wenzake kila kukicha klabuni hapo.

Taarifa zinazoelezwa kwenyo vyombo mbali mbali vya habari huko nchini Uingereza ni kwamba Luca Modric anapigiwa upatu wa kusajiliwa na klabu ya Man Utd kwa lengo la kuziba nafasi itakayoachwa wazi na Paul Scholes.

No comments:

Post a Comment