Monday, February 21, 2011

AS ROMA YAMTENGEA NAFASI ANCELOTTI.

Aliyekuwa Kocha wa AS Roma Claudio Ranieri ambaye kibarua chake kimeota nyasi hivi karibuni.

ROMA, Italia
UONGOZI wa klabu ya AS Roma umemuingiza meneja wa sasa wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti kwenye mipango ya kukirihthi kiti kilicho wazi klabuni hapo.

Uongozi wa klabu ya AS Roma umemuweka Carlo Ancelotti kwenye mikakati hiyo kufuatia hali mbaya inayomkabili kwa sasa huko Stamford Bridge baada ya kikosi chake kusalia na ndoto za kutwaa ubingwa wa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya pekee msimu huu.

Katika kuhakikisha utaratibu huo hauharibu mipango ya Anceloti kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Uongozi wa AS Roma tayari umeshamteua Vincenzo Montella kuwa meneja wa muda, ambapo kibarua hicho atakishikilia hadi mwishoni mwa msimu huu, huku shughuli yake ya kwanza ikitarajiwa kuwa siku ya jumatano katika mchezo wa ligi dhidi ya Bologna huko Stadio Dall'Ara.

Wakati mipango hiyo ikipangwa huko mjini Roma nchini Italia, huko London nchini Uingereza mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich hii leo alitarajiwa kufanya mazungumza na John Terry pamoja na Branislav Ivanovic kwa ajili ya kufahamu nini kinachopelekea mwenendo mbovu ndani ya kikosi chao.

Kama itakumbukwa vyema mapema hii leo meneja wa klabu ya Chelsea Ancelotti amekataa kujiuzulu na badala yake akatangaza kuiweka hatma yake mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Msimamo huo wa kutokua tayari kujiuzulu, ameutoa akiwa safarini kuelekea mjini Copenhagen nchini Denmark tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya FC Copenhagen ya nchini Denmark.


No comments:

Post a Comment