LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amekataa kujiuzulu na badala yake ametangaza kuiweka hatma yake mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
Ancelotti amegoma kujiuzulu nafasi ya umeneja klabuni hapo kufuatia mambo kuendelea kuwa mabaya kwa upande wake huku mashabiki wakimtaka awaachie klabu yao na kurejea nyumbani nchini Italia.
Msimamo wa kutokua tayari kujiuzulu, umetolewa na meneja huyo kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema hafikirii kufanya hivyo kwani bado anaona kuna nafasi ya kuiwezesha Chelsea kufanya vyema katika michuano waliyosalia.
Shinikizo kwa Ancelotti la kuondoka klabuni hapo kutoka kwa mashabiki limejitokeza mara baada ta kikosi chao kushindwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la FA baada ya kukubalia kisago kutoka kwa Everton kupitia changamoto ya mikwaju ya penati 4 dhidi ya 3.

No comments:
Post a Comment