LONDON, England
HOFU kubwa imetanda kwenye kambi Kalusha Bwalya ambae anawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika CAF katika ukanda wa kusini mwa bara la Afrika.
Hofu hiyo imezuka huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huko mjini Khartoum nchini Sudan ambapo Bwalya ametoa angalizo kwa wapiga kura kwa kuwaeleza kwamba wanatakia kutazama namna ya kuendeleza soka ndani ya ukanda huo.
Bwalya ambae alikua mchezaji bora wa barani Afrika mwaka 1988 amesema endapo wajumbe watashindwa kumchagua mtu sahihi kuna uwezekano mkubwa wa soka la ukanda wa kusini mwa bara la Afrika likaendelea kudumaa kama ilivyo sasa ambapo hali hiyo inasababishwa na utawala mbovu ambao hautakiwi kuvumiliwa hata kidogo.
Amesema kimtazamo ukanda wa kusini mwa bara la Afrika ndio kuna wagombea wengi kuliko ukanda wowote wa barani humo hivyo busara na maamuzi ya haki ndio vinavyotakiwa siku ya upigaji wa kura.
Wanaowania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa CAF katika ukanda wa kusini mwa bara la Afrika ni Adam Mthetwa (Swaziland), John Muinjo (Namibia), Justino Fernandes (Angola), Walter Nyamilandu (Malawi) Suketu Patel (Sheli sheli) pamoja na Kalusha Bwalya (Zambia)
Kalusha Bwalya pia anawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA kutoka ukanda huo ambapo katika sehemu hii atapambana na Danny Jordaan (Afrika Kusini) pamoja na Suketu Patel (Sheli sheli).
Katika ukanda wa magharibi mwa Afrika upande B, nafasi ya kamati ya ujumbe ya CAF inawaniwa na Kwesi Nyantakyi (Ghana), Anjorin Moucharafou (Benin) pamoja na Hima Souley (Niger).
Ukanda wa kaskazini mwa bara la Afrika nafasi hiyo inawaniwa na Tarek Bouchamaoui (Tunisia) huku Almamy Kabele Camara akiwania nafasi hiyo kwenye ukanda wa Afrika ya Magharibi upande A.
Katika ukanda wa Afrika ya kati Omari Selemani (Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) yeye anajiandaa kumrithi Thierry Kamach (Jamuhuri ya Afrika ya kati) huku ukanda wa Afrika ya mashariki nafasi hiyo inawaniwa na Leodegar Tenga (Tanzania ) pamoja na Celestin Musabyimana ( Rwanda).
No comments:
Post a Comment