MILAN, Italia
SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya (UEFA) limemfungia mchezaji wa AC Milan Gennaro Gatusso mechi nne baada ya kufanya vurugu katika mchezo wa Champions League dhidi ya Tottenham Hotspurs wiki iliyopita katika Uwanja wa San Siro.
Gatusso alikutwa na kosa baada ya kumsukuma Kocha Msaidizi wa Spurs mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa hatua ya mtoano.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 tayari alikuwa amepewa kadi nyekundu na alitakuwa akose mchezo wa marudiano katika Uwanja wa White Hart Lane, kwa maana hiyo atakosa michezo mitano ya Ulaya.
Mchezaji huyo hataweza kucheza katika mashindano hayo tena msimu huu labda kama timu yake hiyo itafikia hatua ya fainali. Kama haitakuwa hivyo adhabu itaendelea katika msimu ujao wa 2011-2012.
No comments:
Post a Comment