KOCHA wa Marceille Didier Deschamps amesema kuwa Man United bado itakuwa timu inayopigiwa chepuo la kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Champions league hata baada ya kutoa suluhu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Stade Velodrome.
Pamoja na kwamba United ilishindwa kupata bao la ugenini katika mchezo huo, Deschamps alieleza wasiwasi wake huo kuwa anadhani timu hiyo ndio inayopigiwa chapuo la kusonga mbele lakini alisisitiza suluhu hiyo sio matokeo mabaya kwa timu yake.
Wakati akihojiwa na Luninga ya ITV Sport kuhusiana na timu gani anadhani inapewa nafasi ya kusonga mbele kufuatia matokeo hayo ya suluhu alisema, "Nafikiri ni Man United. Sio matokeo mabaya kwetu, lakini ni matokeo mazuri kwa Man United.
Kocha huyo pia alisisitiza kuwa anajivunia kikosi chake na anaamini kuwa hakitatoa nafasi kwa United kupata bao kama wanataka kuwatoa katika michuano hiyo.
"Nimefurahishwa na wachezaji wangu kwasababu nafikiri walicheza vizuri," alisema Deschamps.
"Itakuwa ni muhimu katika marudiano Old Traford kutokubali kufungwa tena na labda tukipata nafasi ya kufunga tuitumie."
No comments:
Post a Comment