Thursday, February 24, 2011

"CR7 NI WINGA NA MSHAMBULIAJI." MOURINHO.

MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa hana uhakika kuwa mchezaji wake Cristiano Ronaldo kama ni winga au mshambuliaji, akiamini kuwa anaweza kumudu nafasi zote vizuri.

Kocha huyo raia wa Ureno aliongea hivyo katika maahojiano na kituo cha Sky Sport, ambapo walikuwa wakiongelea uwepo wa CR7 katika mipango yake, na pia kuhusiana na kuifunga Barcelona nje na ndani.

Akiongea kwa mara ya kwanza kuhusiana na mchezaji huyo, Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter alisema, " Tumejaribu kutafuta nafasi inaweza kumfaa Cristiano, na siku zote kunakuwa na mdahalo katika hilo. Ni mshambuliaji? Sidhani. Nafikiri ni mchezaji aneyeweza kupamba na moja kwa moja na adui.

"Ni Winga? Hapana, kwasababu pia mfungaji na kama ni winga ni magoli mangapi unaweza kufunga katika msimu? nafikiri ni mchanganyiko wa vitu vyote hivyo viwili. Yuko fiti na amekomaa kama mchezaji. Ana kila kitu."

CR7
Kocha huyo pia aliongelea jinsi wachezaji wake walivyochulia kipigo cha mabao 5-0 na barcelona, na alikiri kuwa ingawa ilikuwa ni vigumu kuondoa kichwani tukio lile lakin i wachezaji wake walifanikiwa kuliondoa tukio lile vichwani mwao.

"Kila mtu alikuwa amepagawa, nakumbuka katika mchezo uliofuata dhidi ya Valencia, siwezi kusema kwamba watu walikuwa wanaogopa, lakini walikuwa hawajiamini. Ni jambo la kawaida baada ya kipigo kama kile, lakini wachezaji walifanikiwa kushinda hilo.

"Tunahitaji kuendelea kushinda kama tunavyofanya hivi sasa. Msimu huu tuna kundi la vijana wadogo katika historia ya klabu hii, na naamini kuwa tunafanya vizuri ingawa tunahitaji kushinda chochote."

Mwisho, wakati akiulizwa kama atamaliza mkataba wa miaka minne akiwa Santiago Bernabeu hakuwa na majibu kuhusu hilo, alisema "Sijui. Niliipenda Chelsea, na wakati nikiwa London nilikuwa nafuraha. Nilifikiri nitakuwa pale kwa maisha yangu yote, na miiezi michache nikaondoka. Hivyo siwezi kujua. kama kila kitu kitakwenda sawa nitabaki.

No comments:

Post a Comment