Thursday, February 24, 2011

"WEMBLEY UKO TAYARI KWA AJILI YA FAINALI KOMBE LA LIGI." MKURUGENZI.

Wembley Stadium

LONDON, England
MKURUGENZI Mtendaji wa Uwanja wa Wembley, Roger Maslin amezihakikishia timu za Arsenal na Birmigham kuwa nyasi katika uwanja huo ziko katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa fainali wa Kombe la Ligi baina ya timu hizo.

Kumekuwa na minong'ono kuhusiana na ubora wa nyasi, baada ya Kocha wa Man United Sir Alex Ferguson kusema kuwa mchezaji wake Michael Owen aliumia katika Uwanja huo msimu uliopita kutokana na nyasi hizo kuwa chini ya kiwango, wakati Kocha wa Tottenham Harry Redknapp pia alilalamikia suala kama hilo wakati timu yake ilipofungwa na Portsmouth katika Kombe la FA.

Wembley kwa ndani.
Lakini Maslin alisisitiza kuwa nyasi za uwanja huo ziko katika ubora wa hali ya juu kwa ajili ya mchezo wa huo wa fainali ya Kombe la Ligi.

"Hakutakuwa na tatizo la kupoteza mipira wala kuteleza kwakuwa kuna mabadiliko yalifanywa katika nyasi hizo." alisema Maslin akiambia BBC Sport.

No comments:

Post a Comment