Wednesday, March 16, 2011

ALEX SONG NJE KIKOSI CHA CAMEROON.

Kocha wa Cameroon Javier Clement.

YOUNDE, Cameroon
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon Javier Clemente amemjumuisha kikosini kipa wa klabu ya Espanyol ya nchini Hispania Idriss Kameni huku akimtema kiungo wa klabu ya Arsenal Alex Song pamoja na Achille Edzimbi wa klabu ya Real Betis.

Kocha huyo pia ametangaza kumtema beki wa kushoto wa klabu ya Tottenham Hotspur Benoit Assou-Ekotto huku akimchukua Abouna Ndzana, Julien Momasso pamoja na Andre Ndam Ndam wanaocheza ligi ya nchini Cameroon sambamba na mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya Inter Milan Samuel Eto'o Fils.

Kocha huyo wa kimataifa toka nchini Hispania ametangaza kikosi chake tayati kwa mchezo wa mwishoni mwa mwezi huu ambao utamkutanisha na timu ya taifa ya Senegal kwenye harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika mwaka 2012.

Makipa: Guy Roland Ndy Assembe (Nantes, France), Idriss Kameni (Espanyol, Spain), Charles Itandje (Atromitos, Greece)

Mabeki: Sebastien Basson (Tottenham Hotspur, England), Gaëtan Bong (Valenciennes, France), Benoit Angbwa (Anzhi Makhachkala, Russia), Jean-Patrick Ndzana Abouna (Astres Douala), Nicolas Nkoulou (Monaco, France), Henri Bedimo (Lens, France), Stephane Mbia (Marseille, France)

Viungo: Matthew Mbuta Andongcho (Crystal Palace Baltimore, USA), Enoh Eyong Takang (Ajax Amsterdam, Netherlands), Landry Nguemo (Nancy, France), André Ndam Ndam (Coton Sport), Julien Momasso (Astres Douala), Aurélien Chedjou (Lille, France), Georges Mandjeck (Rennes, France), Benjamin Moukandjo (Monaco, France)

Washambuliaji: Eric-Maxim Choupo Moting (Hamburg, Germany), Somen Tchoyi (West Bromwich Albion, England), Achille Webo (Mallorca, Spain), Samuel Eto'o (Inter Milan, Italy), Vincent Abubakar (Valenciennes, France)

No comments:

Post a Comment