Wednesday, March 16, 2011

CAPELLO KUONGEA NA FERDINAND KUHUSU KUMREJESHEA UNAHODHA TERRY.

LONDON, England
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello anatarajia kukutana na beki wa klabu ya Man Utd Rio Ferdinand kwa ajili ya kumfahamisha maamuzi atakayoyachukua ya kumteua nahodha wa kikosi chake ambacho kitarejea shughulini mwishoni mwa juma lijalo.

Capello anatarajia kufanya mkutano huo saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya huko Old Trafford ambapo wenyeji Man Utd watawakaribisha Olympique de Marseille kutoka nchini Ufaransa.

Capello anategemea kumrejeshea unahodha beki wa klabu ya Chelsea John Terry hivyo ameona ni bora akafanya mazungumzo na Ferdinand ambae hatojumuishwa kikosini kufuatia kuwa majeruhi kwa sasa.

Suala la kurejeshewa unahodha kwa Terry liliibuka jana mara baada ya kocha huyo wa kimataifa toka nchini Italia kufanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alieleza wazi kwamba hana budi kufanya hivyo kutokana na mazingira yaliopo.

Alisema kimtazamo kikosi chake kwa sasa hakina mchezaji mwenye uzoefu wa kuwaongoza wengine zaidi ya Terry ambae alipokonywa unahodha baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu wa kutembea na aliekua rafiki wa mchezaji Wayne Bridge suala ambalo lilizua tafrani katika jamii ya nchini Uingereza.

Mbali na kutarajia kufanya mazungumzo na Ferdinand, Fabio Capello kesho anatarajia kufanya hivyo kwa Terry kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa barabni Ulaya kati ya Chelsea dhidi ya Fc Copenhagen ya nchini Denmark.

Pia mzee huyo wa kitaliano mwenye umri wa miaka 64 atafanya mazungumzo na nahodha msaidizi kwa sasa kwenye timu ya taifa Steven Gerrard siku la Al-khamis kabla ya mchezo wa ligi ya barani Ulaya kati ya Liverpool dhidi ya Fc Bragha.

Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kuwapasha habari wachezaji hao kufuatia maamuzi anayotaka kuyafanya ambayo anaamini yatakubaliwa na wote kwa moyo ulio thabit, tena kwa kuendeleza gurudumu la kikosi cha Uingereza ambacho kitashuka dimbani kucheza na timu ya taifa ya Wales kwenye mchezo wa kuwani nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012.

Hata hivyo maamuzi hayo tayari yameshaanza kupigwa na baadhi ya mashabiki wa soka nchini Uingereza ambapo wamesikika wakidai kwamba Terry hastahili kurejeshewa unahodha kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyeshwa katika jamii.

Madai hayo yamejibiwa na Fabio Capello ambapo alisema anaimani adhabu ya mwaka mmoja aliyoipata mchezaji huyo imetosha na katu hadhani kama anaweza kurejea tena kwenda kinyume na maadili ya jamii inayomzunguuka.

No comments:

Post a Comment