![]() |
Johan Djourou akitolewa nje baada ya kuumia bega katika mchezo dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki. |
LONDON, England
BEKI wa kimataifa toka nchini humo pamoja na klabu ya Arsenal Arsenal Johan Djourou huenda akarejea tena uwanjani kabla ya msimu huu kumalizika kufuatia taarifa njema zilizotolewa mpema hii leo na chama cha soka cha nchini Uswiz.
Mwishoni mwa juma lililopita ilielezwa kwamba Djourou hatorejea tena uwanjani katika kipindi cha msimu kilichosalia, kufuatia kuvunjika bega kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Man Utd lakini imebainika kwamba mchezaji huyo hakuumia kama ilivyokua ikidhaniwa na wengi.
Taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao wa chama cha soka nchini Uswiz zimeeleza kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 24 tayari ameshafanyiwa vipimo na imebainika kwamba jeraha linalomkabili linaweza kutibika kwa siku kadhaa hatua ambayo huenda ikamfanya ajumuishwe kwenye kikosi cha nchi hiyo ambacho mwishoni mwa juma lijalo kitashuka dimbani kucheza mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya dhidi ya timu ya taifa ya Bulgaria.
Hata hivyo kabla ya kutolewa kwa taarifa hizo za chama cha soka nchini Uswiz tayari Djourou alikua ameshathibitisha kwenye vyombo kadhaa vya habari kwa kusema kwamba anaendelea vyema na anahisi huenda akarejea tena uwanjani kabla ya msimu kumalizika.
Kuumia kwa beki huyo kulizusha hofu ndani ya kikosi cha klabu ya Arsenal ambacho kwa sasa kinawategemea mabeki wawili wa kimataifa toka nchini Ufaransa Laurent Koscielny pamoja na Sebastien Squillaci huku Thomas Vermaelen ikiwa bado haifahamiki ni lini atarejea tena uwanjani.
No comments:
Post a Comment