TIMU ya Arsenal wapo kwenye harakati za mwisho za kutaka kumrejesha kikosini aliekua kipa namba moja wa klabu hiyo Jens Lehmann.
Jens Lehmann mwenye umri wa miaka 41 anafikiriwa kurejeshwa klabuni hapo kufuatia tatizo la makipa lililojitojkeza siku za hivi karibuni hali ambayo imekiacha kikosi cha Arsenal kusaliwa na kipa mmoja Manuel Almunia Rivero.
Kipa Wojciech Szczesny yupo nje ya uwanja kufuatia kuvunjika kidole na itamchukua muda wa majuma sita kurejea tena, Lukasz Fabianski amevunjika bega hivyo hatocheza tena hadi msimu ujao huku Vito Mannone akitolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Hull City ambapo hata hivyo nae kwa sasa ni mgonjwa.
Kipa huyo wa kimataifa toka nchini Ujerumani yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu ya Arsenal na endapo mazungumzo hayo yatakamilika kama yanavyotarajiwa huenda akajumuishwa kwenye kikosi kitakachofunga safari mwishoni mwa juma hili kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya West Bromwich Albion utakaopigwa huko The Hawthorns.
Jens Lehmann anakumbukwa na wengi ndani ya klabu ya Arsenal ambayo aliitumikia kuanzia mwaka 2003 hadi 2008 huku akicheza michezo 199.
No comments:
Post a Comment