Wednesday, March 16, 2011

DAN ALVES KUTIMKIA MANCHESTER CITY.

BARCELONA, Hispania
BEKI wa kulia wa klabu bingwa nchini humo Fc Barcelona Daniel Alves huenda akaondoka klabuni hapo kufuatia kuchoshwa na masimango ya kubaguliwa kutokana na rangi ya mwili aliyonayo.

Alves anafikiria kuondoka mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuchoshwa kuitwa nyani na mashabiki wa klabu mbali mbali pamoja na baadhi ya wananchi wa nchini Hispania ambao hukutana nao anapokua matembezini.

Alisema haoni furaha ya kuendelea kuitumikia klabu ya Barcelona iliyomsajili akitokea Sevilla ya nchini humo mwaka 2008 hivyo anafikiri kusaka maisha katika nchi nyingine ambayo anaona itakua afadhali kwake kuishi pamoja na familia yake ambayo pia imekua ikibaguliwa.

Alisema anafikiria kujiunga na klabu ya Man city ambayo ipo tayari kufanya hivyo na imani yake yamtuma maisha ndani ya klabu hiyo huenda yakawa mazuri zaidi ya nchini Hispania ambapo mashabiki walishawahi kumtupia ndizi akiwa uwanjani kwa kumthibitishia hana tofauti na nyani.

Sababu nyingine inayotajwa kumkimbiza beki huyo huko Camp Nou ni ucheleweshaji wa kusainishwa mkataba mpya hatua ambayo ameipokea kama dharau kutoka kwa viongozi wa klabu ya Barcelona ambao walimsajili kwa kitita cha paund za kiingereza million 25.

No comments:

Post a Comment