![]() |
Wembley Stadium. |
LONDON, England
POLISI nchini Uingereza limetoa duku duku lake kufuatia timu pinzani za mjini Manchester kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la chama cha soka nchini humo FA.
Duku duku hilo la polisi limetoka huku ikikadiwa kwamba mchezo huo utakaowakutanisha mahasimu hao ambao ni Manchester United dhidi ya Manchester City April 16 utagharimu kiasi kikubwa cha fedha katika suala la usalama wa mali zilizopo ndani na nje ya Uwanja wa Wembley.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imeeleza kwamba mashabiki wasiopungua elfu 90 wanatarajiwa kuelekea jijini London siku hiyo na hivyo italilazimu jeshi hilo kufanya jitihada zote za kuhakikisha hakutokei hali ya uvunjifu wa amani katika mitaa yote ya jiji hilo.
Kingine kinachozua hofu ni mchezo wa Arsenal dhidi ya Liverpool ambao pia utachezwa jijini London mnamo April 17 sambamba na michuano ya mbio ndefu yaliyopachikwa jina la London Marathon hivyo bado suala la usalama wa hali ya juu litahitajika siku hiyo.
Kufuatia hofu hiyo jeshi la polisi nchini Uingereza limeomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa chama cha soka nchini humo FA kuhakikisha hali ya usalama inatazamwa kwa macho mawili kwa kutoa mamilion ya paund yanayotarajiwa kupotea kama posho kwa askari wa jeshi hilo watakaomwagwa jijini.
Mchezo mwingine wa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la FA utakua kati ya Stoke City dhidi ya Bolton Wanderers ambapo utachezwa April 17 kwenye uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment