Friday, March 18, 2011

CHELSEA, MAN UNITED KUVAANA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE, TOTTENHAM NA KIBARUA KIZITO DHIDI REAL MADRID.

LONDON, England
MANCHESTER United na Chelsea zitakutana katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Champions League iliyopangwa mchana huu.

Vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza United, ambao waliwafunga Chelsea kwa matuta jijini Moscow katika fainali ya michuano hiyo watakuwa wamefurahia droo hiyo kwa kuwa wataanza kucheza ugenini na kumalizia nyumbani dhidi ya Chelsea.

Tottenham wenyewe wataikwaa Real Madrid. Ingawa na wenyewe watacheza mchezo wa pili wakiwa nyumbani.

 Barcelona wenyewe wamepangwa na timu mchekea Shakhtar Donetsk ya Ukraine wakati mabingwa watetezi wa michuano hiyo Inter watacheza na Schalke 04. Ratiba yote ni kama ifuatavyo.

ROBO FAINALI
Real Madrid v Tottenham Hotspurs
Chelsea v Manchester United
Barcelona v Shakhtar Donetsk
Inter Milan v Schalke 04

NUSU FAINALI
Mshindi kati ya Chelsea au Man United atacheza na mshindi kati ya Inter Milan na Schalke 04.
Mshindi kati ya Barcelona au Shakhtar Donetsk atacheza na mshindi kati ya Real Madrid au Tottenham Hotspurs.

No comments:

Post a Comment