Wednesday, March 16, 2011

PAMOJA NA MAAFA YALIYOIKUMBA JAPAN, JFA YATHIBITISHA USHIRIKI WA TIMU HIYO KATIKA MICHUANO YA COPA AMERIKA.

TOKYO, Japan
SHIRIKISHO la Soka la Japan (JFA) limesema kwamba litapeleka timu katika michuano ya Copa Amerika inayotarajiwa kufanyika Argentina pamoja na nchi kuwa katika majonzi ya kukumbwa na tetemeko la ardhi la chini ya bahari hivi karibuni ambapo watu zaidi ya 10,000 wanahofiwa kupoteza maisha.

Katibu Mkuu wa JFA Kozo Toshima alithibitisha ushiriki wa timu hiyo katika mashindano hayo, pamoja na kukabiliwa na wakati huo mgumu.

Kwa kusimamisha Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama J-league hiyo mpaka mwezi April, hiyo inamaanisha ligi hiyo ya nyumbani itaendelea wakati wa michuano ya Copa Amerika.

Kikosi cha uokoaji kikipita katika mabaki ya nyumba za watu  ya mji wa Ofunano nchini Japanmara baada ya tetemeko hilo la chini ya bahari (Tsunami) kutokea na kusababisha mawimbi makubwa ambayo yaliharibu pamoja na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, tetemeko hilo linakadiriwa kuwa na kipimo cha 8.9 magnitude.
Hali hiyo inamaanisha kuwa vilabu vitawakosa nyota wake kama wakiitwa katika timu ya Taifa, au watapeleka kikosi dhaifu katika michuano hiyo.

Kocha wa Japan Alberto Zaccheroni ataweza kulazimika kuita nyota wa timu hiyo waliopo Ulaya ili kuinusuru J-League kuwakosa nyota wake.

No comments:

Post a Comment