Wednesday, March 16, 2011

FERGUSON ALA KIBANO CHA MECHI TANO.

LONDON, England
SHIRIKISHO la Soka nchini Uingereza (FA) limemfungia mechi tano Kocha wa timu ya Manchester United Sir Alex Ferguson ikiwemo mchezo wa nusu fainali ya FA Cup dhidi ya mahasimu wao Manchester City.

Shirikisho hilo lilimkuta Ferguson na makosa kwa kumtolea maneno ya kashfa mwamuzi Martin Atkinson katika mchezo dhidi ya Chelsea ulifanyika Stamford Bridge.

Mwamuzi huyo alitoa penati katika mchezop huo ambayo Frank Lampard alifunga na kuipa ushindi timu hiyo katika mchezo huo.

Ferguson pia ametozwa faini ya paundi 30,000 kwa tukio hilo na FA imempa masaa 48 ya kukata rufaa.

No comments:

Post a Comment