![]() |
Kutoka kulia Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura, Kocha wa Taifa Stars Jan Poulsen pamoja na wawakilishi wa wadhamini wa timu hiyo kutoka Serengeti na NMB wakizungumza na waandishi wa habari. |
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kitakachovaana na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kati katika mechi itakayofanyika Machi 26 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni wa kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea hapo mwakani.
Poulsen amekitaja kikosi hicho kuwa ni magolikipa ni Shaban Kado(Mtibwa Sugar), Juma Kaseja (Simba) na Shaaban Dihile (JKT Ruvu).
Mabeki ni pamoja na Shadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Stephano Mwasika (Yanga), Haruna Shamte (Simba), Juma Nyoso (Simba) na Idrissa Rajab (Sofapaka-Kenya).
Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz (Azam), Henry Joseph (Kongsvinger IL-Norway), Abdi Kassim (DT Long An-Vietnam), Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni Dan Mrwanda (DT Long An-Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps-Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mohamed Banka (Simba), Athuman Machupa (Vasalund IF-Sweden), John Bosco (Azam) na Mbwana Samata (Simba).
Katika msimamo wa kundi D Stars iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja iliyoipata baada ya kutoka sare na Algeria.
No comments:
Post a Comment