Monday, March 7, 2011

"LIVERPOOL IKO JUU." KUYT.

LONDON, England
MFUNGAJI wa mabao matatu katika mchezo wa jana kati ya Liverpool dhidi ya Man Utd Dirk Kuyt alisema kuna nafasi kubwa ya klabu yake kufikia malengo yaliyowekwa msimu huu kufuatia kuwa na safu nzuri ya wachezaji.

Dirk Kuyt aliepachika mabao matatu pekee yake ambayo yaliizamisha Man utd jana jioni alisema safu ya wachezaji iliopo klabuni hapo itakua chachu tosha kwa kikosi kizima cha klabu ya Liverpool kuendelea kufanya maajabu zaidi ya yale yaliyoonekana katika mchezo wa jana.

Alisema ujio wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Alberto Sularez Diaz pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Andy Carroll kumeongeza chachu ya kujituma kwa kila mmoja ambae ana uchungu wa kutotaka kuona Liverpool hairejei yale waliyoyafanya msimu uliopita.

Alisema mchango mkubwa ulioonyeshwa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Sularez katika mchezo wa jana umewapa imani wao kama wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kuwa kuna kila linalowezekana mbele yao kabla ya kumalizika kwa msimu huu, huku pia akisifia kiwango cha Andy Carroll.

Ushindi wa mabao matatu kwa moja uliopatikana jana huko Anfiled unaipa nafasi Liverpool kujituliza katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha point 42.

No comments:

Post a Comment