Monday, March 7, 2011

MKEKA KUMKIMBIZA KALOU CHELSEA.

LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Salomon Kalou alisema huenda akaondoka huko Stamford Bridge mwishoni mwa msimu huu endapo ataendelea kukalia mkeka kama ilivyo hivi sasa.

Solomon Kalou ameamua kupasua ukweli huo kufuatia hali mbaya kuendelea klabuni hapo toka mwishoni mwa mwezi Januari aliposajiliwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando Torres akitokea Liverpool.

Kalou, mwenye umri wa miaka 25, ambae alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2006 akitokea nchini Uholanzi kwenye klabu ya Feyenoord amesema amekuwa na wakati mgumu wa kujumuishwa katika kikosi cha kwanza hali ambayo inamkera hivyo anaona njia sahihi ni kuondoka na kwenda kusaka maisha kwingine.

Alisema haoni sababu ya kuendelea kuwekwa benchi wakati bado ana uwezo mkubwa wa kukitumikia kikosi cha kwanza cha klabu ya Chelsea ambacho kinahitaji usaidizi mkubwa katika kipindi hiki baada ya kupotea mwishoni mwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment