Monday, March 7, 2011

NANI AHOFIWA KUTOCHEZA MSIMU WOTE ULIOSALIA.

LONDON, England
WINGA wa kimataifa toka nchini Ureno pamoja na klabu ya Manchester United Luís Nani huenda ikamchukua muda mrefu kurejea tena uwanjani kufuatia rafu mbaya aliyochezewa na beki wa klabu ya Liverpool katika mchezo wa jana Jamie Carragher.

Msemaji wa klabu ya Man Utd alisema winga huyo mwenye umri wa miaka 24 anahofiwa huenda ikamchukua muda mrefu kufutia muonekano wa jeraha alilolipata ambalo lilimlazimu kutolewa nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na Javier Hernández "Chicharito".

Alisema hofu iliyotanda klabuni hapo ni kutokana na jeraha la mchezaji huyo linavyoonekana, na wengi wao wanadhani huenda akawa amepata mpasuko kwenye mfupa wa ugoko wa mguu wake wa kulia lakini bado akasisitizia kwamba hii leo wataujua ukweli baada ya kufanyiwa vipimo.

Hata hivyo pamoja na Nani kuchezewa rafu mbaya bado muamuzi Phil Dowd alimuonyesha kadi ya njano Jamie Carragher.

Katika mchezo huo Man utd waliziacha point tatu muhimu huko Anfiled baada ya kukubalia kisago cha mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment