Monday, March 7, 2011

SONG KUIKOSA BARCELONA.

LONDON, England
KIUNGO wa kimataifa toka nchini Cameroon pamoja na klabu ya Arsenal Alex Song  hii leo ameshindwa kusafiri na kikosi cha klabu yake kuelekea mjini Barcelona kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Alex Song hakujumuika na wenzake safarini kufuatia maumivu ya goti kuendelea kumsumbua hali mbayo itampa nafasi meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kusaka mchezaji mbadala atakaecheza nafazi ya kiungo huyo.

Taarifa za kushindwa kusafikiri kwa Song zimethibitishwa hii leo mchana kwa saa za hapa nyumbani na Wenger ambapo amesema kabla ya maamuzi ya kutojumuishwa safarini hayajachukuliwa kiungo huyo jana alifanyiwa vipimo na kubainika bado anahitaji muda wa kuendelea na matibabu.

Hata hivyo mzee huyo ameonyesha uso wa furaha baada ya kupewa ruhusa ya kumtumia nahodha na kiungo wake Cesc Fàbregas katika mchezo wa kesho kufuatia kupona jeraha la nyama za paja alilolipata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Stoke City.

Alisema kiungo huyo amefanyiwa vipimo na kuonekana yupo fit hivyo kurejea kwake kutaleta changamoto kwa wachezaji wengine kujituma kwa asilimia kubwa kwenye mchezo huo utakaopigwa huko Camp Nou.

Jack Wilshere nae amefanyiwa vipimo na kuonekana yupo sawa sawa kwa ajili ya mchezo huo kufuatia kupata maumivu ya kifundo cha mguu mwishoni mwa juma lililopita pale Arsenal walipokua nyumbani wakicheza na Sunderland na kupata matokeo ya sare.

Taarifa tulizozipokea muda mchezo uliopita zinaeleza kwamba mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Robin van Persie amejumuishwa kwenye kikosi kilichoelekea nchini Hispania hii leo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Barcelona.

Robin van Persie alikua anahofiwa huenda asingejumuika na wachezaji wengine katika safari hiyo kufuatia maumivu wa goti aliyoyapata kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la ligi ya nchini Uingereza *Curling Cup* dhidi ya Birmingham city.

Mapema hii leo mshambuliaji huyo alionekana mazoezi akiwa sambamba na wachezaji wengine na imeonekana yupo fit hivyo mishale ya mchana alijumuishwa kikosini tayari kwa safari.

Kikosi kamili cha Arsenal kilichokwea pipa kwenda Camp Nou ni kama ifuatavyo, Manuel Almunia, Wojciech Szczesny, Johan Djourou, Gael Clichy, Emmanuel Eboue, Kieran Gibbs, Laurent Koscielny, Bacary Sagna, Sebastien Squillaci, Cesc Fabregas, Andrey Arshavin, Jack Wilshere, Tomas Rosicky, Samir Nasri, Abou Diaby, Denílson Pereira Neves, Nicklas Bendtner, Marouane Chamakh pamoja na Robin van Persie.

Kwa upande wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona wao wataingia uwnajani bila ya kuwa na nahodha na beki wao Carles Puyol Saforcada ambae bado anasumbuliwa na maumivu ya gopti la mguu wake wa kushoto.

No comments:

Post a Comment