Tuesday, March 1, 2011

MAN UNITED YAKUBALI KIPIGO DARAJANI, YACHAPWA 2-1 NA CHELSEA.

Mshambuliaji wa Man United Wayne Rooney akipiga shuti ambalo lilizaa bao la kuongoza dhidi ya Chelsea wakati timu hizo zilikutana katika Uwanja wa Stamford Bridge usiku huu. 

Rooney na Luis Nani wakishangilia mara baada ya kufungwa kwa bao hilo.

Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza David Luiz mara baada ya kusawazisha bao katika mchezo huo. 

Kiungo wa Chelsea Frank Lampard akipiga penati baada beki wa Man United Smalling kumfanyia madhambi kiungo Zhirkov katika eneo la hatari. 

Lampard na Didier Drogba wakishangilia mara baada ya mchezaji kuiandikia timu yake bao la pili na kuifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. 

Wachezaji Nani wa Man United na Ivanovic wa Chelsea wakichimbana biti mapema kipindi cha kwanza katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment