Friday, April 1, 2011

MESSI FITI KUIVAA VILLAREAL.

BARCELONA, Hispania
JOPO la madaktari wa klabu ya Barcelona hii leo limekua na kazi nzito ya kumshughulikia kiungo wa kimataifa toka nchini Argentina Lionel Messi kwa lengo la kumuwezesha kucheza mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili.

Jopo la madakrtari huko mjini Catalan limefanya shughuli hiyo ikiwa ni sehemu ya kuongeza chachu ya kusaka ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Hispania ambapo Barcelona mpaka hii leo bado wapo kileleni kwa tofauti ya point tano dhidi ya Real Madrid ambao wana malengo ya kumaliza ukame wa kutwaa taji la nchini humo.

Baada ya kufanyiwa vipimo Messi amebainika kwamba hana tatizo linalomsumbua kama ilivyoripotiwa hapo awali zaidi ya kupata mshtuko wa misulu ya paja alipokua kwenye maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu y taifa ya Argentina dhIdi ya timu ya taifa ya Costa Rica.

Hata hivyo bado kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ataendelea kufanyiwa uchunguzi akiwa mazoezini na wenzake ili kufahamu mustakabali wa hali yake itamruhusu kujumuishwa kikosini mwishioni mwa juma hili pale FC Barcelona watakapowakabili dhidi ya Villarreal.

Mapema hii leo taarifa zilieleza kwamba Messi alikua kwenye mashaka makubwa ya kuukosa mchezo huo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili sambamba na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa kati kati ya juma lijalo dhidi ya Shakhtar Donetsk kutoka nchini Ukraine.

No comments:

Post a Comment